TANGAZA NASI SASA
Thursday, January 10, 2013
PICHA : TUNAWASILISHA MAONI
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Absolom Kibanda
akimkabidhi maoni ya Jukwaa hilo kuhusu katiba Mpya Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini
Dar es Salaam leo
Mwanachama wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus
Balile akiwasilisha maoni ya Jukwaa hilo kuhusu Katiba Mpya katika
mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Bw. Ruge Mutahaba (kushoto)
kutoka Clouds Media Group na Bw. Yasin Sadik kutoka gazeti la Hoja.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Bw. Kajubi Mukajanga akiwasilisha maoni ya Baraza hilo kuhusu Katiba
Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam leo. Kulia ni Bi. Pili
Mtambalike kutoka MCT.
Saturday, December 15, 2012
WAAJIRI BORA WAPATIWA TUZO
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto cheti baada y kuwa mmoja wa
wafadhiri wa hafla ya kuwazawadia waajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City,
Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto akishangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete kumkabidhi
tuzo ya ushindi wa tatu ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla
iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Mlimani City, Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth
Wanyoto cheti baada y kuwa mmoja wa wafadhiri wa hafla ya kuwazawadia waajiri
Bora wa Mwaka 2012 katika hafla
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.Kushoto ni
Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
Wanyoto akipita na tuzo mbele ya Rais Kikwete pamoja na
Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
TAARIFA KUTOKA IKULU
Rais wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina ambaye
amewasili mjini Dar es Salaam mchana jana Ijumaa, Desemba 14 kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili nchini akiwa na
mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, tayari kuanza
mazungumzo rasmi.
Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu
na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar
kuwaelezea maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC uliofanyika mwishoni mwa
wiki mjini Dar Es Salaam.Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
Ikulu, Dar Es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii, Mheshimiwa Ravalomanana
alithibitisha kuwa amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka
viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika
Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani.
Subscribe to:
Posts (Atom)