Rais wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina ambaye
amewasili mjini Dar es Salaam mchana jana Ijumaa, Desemba 14 kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili nchini akiwa na
mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, tayari kuanza
mazungumzo rasmi.
Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu
na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar
kuwaelezea maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC uliofanyika mwishoni mwa
wiki mjini Dar Es Salaam.Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
Ikulu, Dar Es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii, Mheshimiwa Ravalomanana
alithibitisha kuwa amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka
viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika
Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani.
No comments:
Post a Comment